Raia wa Tanzania amefikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la kuwa nchini bila kibali.
Upande wa mashtaka ulielezea mahakama kuwa mshtakiwa, Rashid Nuru, alipatikana katika eneo la Kiziwani, Kaunti ya Mombasa, mnamo tarehe 17 mwezi wa Aprili, bila kibali cha kumruhusu kuwa nchini.
Nuru alikubali shtaka hilo siku ya Jumanne mbele ya Hakimu Susan Shitubi.
Hakimu Shitubi alimtoza kijana huyo faini ya shilingi laki moja au kifungo cha mwaka mmoja jela.
Aidha, Hakimu Shitubi aliagiza mshtakiwa kurudishwa nchini Tanzania baada ya kukamilisha kifungo hicho.