Mshukiwa wa ugaidi Jameine John Grant amefungwa kifungo cha miaka tisa gerezani kwa mashtaka tisa ya kughushi vyeti vya kuzaliwa na vya shule.
Akitoa hukumu hiyo siku ya Jumatano, Jaji Martin Muya alisema kuwa hukumu hiyo itakuwa funzo kwa wengine wanaojihusisha na tabia ya kughushi vyeti.
Grant, ambaye ni raia wa Uingereza, anadaiwa kughushi stakabadhi hizo kati ya Septemba 19,2012 na 26,2012 katika eneo la Kisauni.
Haya yanajiri baada ya afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma kukata rufaa ya kupinga uamuzi wa mahakama ya chini ya Shanzu iliyomwondolea mashtaka hayo mshukiwa huyo.
Jaji Muya aliongeza kuwa mahakama ya Shanzu haikuzingatia ushahidi muhimu uliotolewa na mashahidi wa kesi hiyo, hivyo basi ilipendelea upande mmoja.
Grant yuko na siku 14 za kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.
Grant anakabiliwa na mashtaka mengine ya ugadi na kuwa na uhusiano wa kigaidi na kundi la Al-shabab.