Raia wawili wa Ujerumani wamefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la kujaribu kusafirisha miraa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mahakama ilielezewa siku ya Jumatatu kuwa washukiwa hao, Vadims Federonkos na Nader Moussa, wanadaiwa kupatikana na kilo 55 ya miraa aina ya mogoka yenye thamani ya shilingi 50,000, katika uwanja wa ndege wa Moi mnamo Machi 3, 2016.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa wawili hao walikuwa na lengo la kusafirisha miraa hiyo hadi nchini Ujerumani kinyume cha sheria.

Wawili hao walikubali mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkuu Susan Shitub.

Vadims Federonkos alitozwa faini ya shilingi 17,250 naye Nader Moussa akatozwa faini ya shilingi 10,000 ama wote watumikie kifungo cha miezi mitatu kila mmoja.