Raia wa Yemen, anayekabiliwa na shtaka la ugadi, atazuiliwa kwa siku tano zaidi ili kusubiri uchunguzi dhidi yake kukamilika.
Haya yanajiri baada ya upande wa mashtaka kuomba muda zaidi wa kukamilisha uchunguzi wake.
Waleed Ahmed Mohamed, alitiwa mbaroni Agosti 11, 2016 katika eneo la Kivuko cha feri cha Likoni baada ya kuhusishwa na kundi la kigaidi.
Vyeti vya mshukiwa huyo vinaonyesha kuwa alikuwa mwanajeshi wa umoja wa ulaya nchini Yemen, anayedaiwa kutoroka jeshi hilo kutokana na vita.
Hakimu Daglous Ogoti alikubali ombi hilo siku ya Jumatatu na kuagiza mshukiwa huyo kuzuiliwa kwa siku tano zaidi.
“Nakubaliana na ombi la upande wa mashtaka la kumzuia Waleed kwa siku tano zaidi,” alisema Hakimu Ogoti.
Kesi hiyo itatajwa Agosti 19, mwaka huu.