Mahakama ya Mombasa imemuachilia huru raia wa Yemen aliyekuwa anakabiliwa na tuhuma za ugaidi.
Waleed Ahmed Mohammed alitiwa mbaroni wiki iliyopita katika kivuko cha feri cha Likoni baada ya kuhusishwa na kashfa za ugaidi.
Uchunguzi uliofanywa umeonyesha kuwa Waleed hana uhusiano wowote na kundi la kigaidi bali alihudumu kama askari wa kampuni ya usalama ya kibinafsi nchini Yemen.
Aidha, uchunguzi huo unaonyesha kuwa Waleed anauzoefu wa kutumia silaha kama vile bunduki, ikizingatiwa walinzi wa kampuni za kibinafsi nchini Yemen hupewa mafunzo ya kijeshi ikiwemo kutumia silaha.
Siku ya Ijumaa, upande wa mashtaka pamoja na maafisa wa kupambana na ugaidi ATPU waliiomba mahakama kumuachilia huru Waleed baada ya uchunguzi kukaamilika.
Hakimu Daglous Ogoti alikubali ombi hilo na kuagiza jamaa huyo kurudishwa nchini Yemen.
Mikakati ya kumrudisha Waleed nchini Yemen imeanza kufuatia agizo la mahakama.