Maafisa wa polisi katika gatuzi dogo la Likoni wamewatia mbaroni raia watano wa Ethiopia waliokuwa humu nchini kinyume cha sheria.
Kulingana na mkuu wa polisi eneo la Likoni Willy Simba, watano hao walikamatwa baada ya polisi kupashwa habari na wananchi kuhusu uwepo wa raia hao katika eneo la Makao Mema, huko Majengo Mapya.
Watano hao, Habib Mohamed, Bilal Kimbado, Matheus Godebo, Dasane Bako na Tamaskei Malaso, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumatano.