Kinara wa upinzani na kiongozi wa mrengo wa Cord, Raila Odinga amelaumu serikali ya Jubilee kwa kufeli kupitishwa kwa mswaada muhimu kuhusu uakilishi wa angalau tuluthi moja katika bunge la kitaifa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mswaada huo ulifeli baada ya wabunge 179 kuunga mkono, kinyume na idadi ya wabunge 233 iliyohitajika mswaada huo kupita.

Muungano wa wabunge wanawake umesema utashinikiza mswaada huo kurejeshwa bungeni na kupitishwa. Inabainika kuwa serikali haitaki mswaada huo kupitishwa ili kuleta uakilishi sawa katika mbunge la kitaifa na lile la seneti.

Iwapo mswaada huo hautapitishwa kufikia mwezi Agosti, inaaminika kuwa mkenya yeyote anaweza kwenda mahakamani na kuiomba mahakama kuvunjilia mbali mbunge kwa kuwa wambunge wamefeli kupitisha mswaada muhimu katika katiba ya Kenya.

Kufeli kwa kupitishwa mswaada huo inaadhihirisha kuwa wabunge hawaheshimu katiba.

Mswaada huo unatarajiwa kurejeshwa mahakamani tena hii ikiwa ni mara ya pili mswaada huo ulikosa kupitishwa mbungeni.