Aliyekuwa mwenyekiti wa TNA tawi la Nakuru Dkt Abdul Noor, amemtaka rais Uhuru Kenyatta kufanya mazungumzo na vinara wa Cord, ili kuzuia ghasia kuweza kuchipuka kutokana na misururu ya maandamano unaotekeleza muungano huo ya kushinikiza tume ya IEBC kung’atuka afisini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza na mwandishi huyu Jumatatu kwa njia ya simu akiwa jijijni Nairobi, Noor alishangazwa na idadi kubwa ya maafisa wa usalama waliokuwa wakilinda doria jijini humo kuzuia ghasia kuzuka katika mandamano yanayoandaliwa na muungano wa CORD.

"Ikiwa muungano huo hautasikizwa na kuendeleza maandamano hayo, huenda Kenya ikapoteza wawekezaji wa kigeni na hhatua hiyo itadidimiza uchumi wa nchi," aliongeza Noor.

Ameongeza kuwa taifa la Kenya huenda likaadhirika kiuchumi na kufufuka kwake huenda litakuwa baada ya uchaguzi mkuu ujao mwakani 2018.

Amesema kuwa vinara wa muungano huo wanafaa kupewa nafasi ya kupeleka malalamishi yao kwenye afisi za tume ya IEBC ili kuleta hali ya utulivu nchini.

Amesema kama wakenya tunahitaji amani sasa na siku zijazo.