Wito unazidi kutolewa kwa rais Uhuru Kenyatta pamoja na naibu wake William Ruto kutumia uhuru wao baada ya kuporomoka kwa kesi za ICC kuwatafutia haki waathiriwa ghasia za baada ya Uchaguzi mkuu wa 2007/008. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanaharakati wa kutetea haki za kijamii Shaffie Hussein Ali alisema waathiriwa hao wanastahili kupewa makao mbadala au kufidiwa, hatua anayosema itawapa nafasi ya kurejelea hali yao ya maisha sawa na Wakenya wengine.

“Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wanafaa kuchukuwa jukumu la kuwapa angalau haki hata kama si kikamilifu kwa waathiriwa ikilinganishwa kuwa wao wameshaondolewa lawama ila waathiriwa nao bado wapo na machungu mengi,” alisema Shaffie.

Mwanaharakati huyo vile vile alitaka kutekelezwa kikamilifu wa ripoti ya iliyokuwa tume ya haki, ukweli na maridhiano ili kushughulikia dhulma za kihistoria zilizotokea miaka iliyopita.

“Mapendekezo ya ripoti ya TJRC yashughulikiwe kama njia moja wapo ya kuwatuliza wakenya hasaa wakati huu ambapo tuanelekea katika uchaguzi mkuu mwingine wa mwaka 2017,” aliongeza Shaffie.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ugatuzi na Mipango Mwangi Kiunjuri, serikali inaendelea na mipango ya kutathmini uhalali wa wakimbizi walioathirika na ghasia za baada ya Uchaguzi mkuu wa 2007/008 ikiwa na madhumuni ya kuwapa makao mbadala.