Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mashirika yakijamii kutoka Bonde la Ufa yamemtaka Rais Uhuru Kenyatta kutoweka saini kwenye sheria tata ya vyombo vya habari. 

Mashirika hayo yamesema sheria hiyo ambayo ilipitishwa bungeni inalenga kudhulumu wanahabari na uhuru wa vyombo vya habari kwa jumla.

Kulingana na mashirika hayo, iwapo rais ataweka saini kwenye sheria hiyo, atakuwa anarejesha Kenya katika enzi za giza na utawala wa kiimla.

Mkuruganzi wa kituo cha haki za kibinadamu na Maendeleo Centre for Human Rights and Democracy, Ken Wafula alitahadharisha rais dhidi ya kuweka saini kwenye mswada husika.

“Kama mashirika ya kijamii tutatumia kila mbinu kupinga sheria hiyo hadi pale kipengele tata ambacho kinatishia uhuru wa waandishi wa habari na vyombo vya habari kitakapoondolewa,” alisema Wafula.

Wafula alisema iwapo rais ataweka saini kwenye sheria hiyo, mashirika hayo yatafika mahakamani kupinga sheria hiyo mbali na kushiriki maandamano.

Msimamo sawa na huo umetolewa na Nick Omito, ambaye ni mkurugenzi wa shirika la Human Rights and Mitigation.

Omito alilaumu wabunge ambao walipitisha mswada huo, na kusema kuwa wamejichimbia kaburi la kuanguka ndani baada ya uchaguzi mkuu ujao.

Mkurugenzi huyo alisema huenda wabunge ambao waliunga mswada huo mkono hawakuelewa walichokuwa wakifanya, au kulikuwa na ufisadi wa aina fulani katika mswada husika.

Nalo bunge la wananchi mjini Eldoret limetishia kuanza kushiriki maandamnao hadi pale rais Uhuru Kenyatta atatangaza kutupilia mbali sheria hiyo.

“Waandishi wa habari wanatetea watu wa chini kama sisi, na kutuonyesha yanayojiri bungeni, sheria hii itatunyima nafasi hiyo,” alisema Naftali Kosgei, mmoja wa viongozi wa bunge hilo.

Kosgei alisema bunge hilo litaanza kukusanya saini za kutaka bunge kuvunjwa ili wabunge ambao hawaelewi majukumu yao warudi nyumbani.

Wanachama wa bunge la mwananchi mjini humo walidai kuwa wabunge wa bunge la sasa wamezembea zaidi