Rais Uhuru kenyata ameipongeza Bandari ya Mombasa kwa utendakazi wake na kusema kuwa bandari hiyo ni mojawapo ya vigenzo muhimu katika kukuza uchumi humu nchini.
Katika hotuba yake kwa taifa siku ya Alhamisi kwenye Bunge la Kitaifa jijini Nairobi, Rais Kenyatta alisema kuwa bandari hiyo imepiga hatua kutoka kuwa bandari ya nane barani Afrika hadi nambari ya nne.
Rais Kenyatta pia alisema kuwa serikali ya kitaifa itaendelea kuweka mashine za kidijitali bandarini humo, ili kuweza kurahihisha na kupunguza muda unaotumika katika shughuli za upakuzi na upakuaji.
Itakumbukwa kuwa Bandari ya Mombasa imekuwa ikihudumia zaidi ya nchi nne barani Afrika zikiwemo nchi ya Uganda, Sudan Kusini,Burundi na nchi ya Rwanda.