Kufuatia hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kuiachisha kazi bodi ya hazina ya pesa za vijana nchini, katibu mratibu wa chama cha mashamba makubwa makubwa nchini amejitokeza kumpongeza rais Kenyatta kwa hatua aliyochukua.

Share news tips with us here at Hivisasa

"Hatua ambayo rais Uhuru Kenyatta alichukua kwa kuwafuta kazi maafisa wakuu wa hazina ya vijana ni nzuri na inaonyesha wazi kwamba Rais amejitolea kupambana na ufisadi nchini," alisema Omasire. 

Omasire aidha aliwataka maafisa husika wa hazina hiyo kuwajibikia uvujaji wa mamillioni ya pesa kutoka kwa hazina hiyo. 

"Haiwezekani kwamba watu wanapewa kazi ya kusimamia pesa za hazina ya vijana zinazokusudiwa kuwasaidia vijana kuimarisha maisha yao na kisha wanazivuja, na ndio maana sharti wawajibikie vitendo vyao kwa kurejesha mamillioni ya pesa walizozivuja," aliongezea Omasire.