Rais Uhuru Kenyatta ametangaza wazi kwamba serikali ya kitaifa imeweka mikakati ya kuhakikisha shule zote za msingi zimeunganishiwa nguvu za umeme.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiwahutubia wakazi wa Kebirigo kule Nyamira wakati wa ziara yake eneo hilo siku ya Jumatano, Uhuru alisema kuwa serikali yake imefanikisha mradi wa kuunganishia shule zote za msingi umeme. 

"Serikali yangu imeweka mikakati ya kuhakikisha kwamba shule zote za umma nchini zimeunganishiwa umeme, na nina hakika kuwa hamna shule hata moja hapa Nyamira ambayo haijaunganishiwa nguvu hizo za umeme," alisema Kenyatta. 

Kenyatta aidha aliongeza kwa kusema kuwa tayari serikali ya Jubilee imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa kwa miaka mitatu ijayo kila boma nchini zitakuwa zimeunganishiwa umeme. 

"Tumeweka mipango ya kutaka kuona kuwa kufikia miaka mitatu ijayo thuuthi tatu ya wananchi watakuwa wameunganishiwa nguvu za umeme kwenye boma zao," aliongezea Kenyatta.