Rais Uhuru Kenyatta ameutaka mrengo wa Cord kufata sheria ilioko kwenye katiba kushinikiza mabadikiko kwa Tume huru ya mipaka na uchaguzi IEBC.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza siku ya Alhamisi wakati wa ziara yake huko Mandera, Kenyatta alisema kuwa yeye hana uwezo wa kubandua tume hiyo na sharti sheria kufuatwa.

"Katiba imeweka wazi taratibu zote zinazopaswa kufuatwa kubandua tume hiyo. Maandamano hayawezi kufanikisha agenda ya upinzani,” alisema Kenyatta.

Rais Kenyatta alisisitiza kuwa atazidi kuitetea Katiba kwa vile alichukua kiapo kuilinda.

Kwa upande wake, Naibu wa Rais William Ruto, alisema kuwa wako tayari kushauriana na Cord kuhusu swala hilo.

"Tuko tayari kushauriana na upinzani kuhusu kubanduliwa kwa Tume ya IEBC lakini kwa misingi ya kisheria,” alisema Ruto.

Haya yanajiri huku hisia tofauti zikiendelea kuibuka kuhusu njia mwafaka ya kuleta mabadiliko yafaao katika Tume ya IEBC.