Raisi Uhuru Kenyatta ameitaka serikali ya Kaunti ya Mombasa kushirikiana na serikali kuu katika kuimarisha sekta ya uvuvi ambayo ndio uti wa mgongo wa uchumi kwa wakaazi wa Pwani.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kenyatta amesema kuwa iwapo uvuvi utaboreshwa, basi vijana wengi wa eneo la Pwani watapata ajira na kujikimu kimaisha.

“Uvuvi ukiweza kuimarishwa basi idadi kubwa ya vijana wataweza kujiajiri wenyewe na kuimarisha uchumi wa Pwani na taifa kwa jumla,” alisema Uhuru.

Akizungumza siku ya Alhamisi wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kilimo, Rais Kenyatta aliahidi kuboresha sekta hiyo kwa kutoa ngarawa na maboti kwa wavuvi ili kuendeleza sekta hiyo.

“Bado wavuvi wetu wanatumia vifaa duni kabisa, ndio maana hawashiki samaki wengi,” alisema Kenyatta.

Rais Kenyatta pia ameitaja sekta ya uvuvi kama iliyodorora na kutofaidi taifa kwa muda mrefu.

“Uvuvi haujaleta faida yoyote kwa taifa hili. Haya yote yanaletwa na vifaa duni ambavyo vinatumiwa na wavuvi wetu baharini,” alisema Kenyatta.