Rais Uhuru Kenyatta amempongeza aliyekuwa komanda wa wanajeshi Generali Geoffrey Obwoge kwa kujitolea kutetea taifa la Kenya na kupambana na magaidi wa al-Shabaab nchini Somalia.
Obwoge aliuawa kwenye shambulizi lililotekelezwa na kundi hilo la magaidi wa al-Shabaab mnamo Januari 15 mwaka huu na kusababisha baadhi ya wanajeshi wa Kenya kupoteza maisha yao huku komanda Obwoge akiwa mmoja wao.
Generali Walter Ralia alisoma ripoti ya Uhuru Kenyatta kwenye mazishi ya marehemu Obwoge kwenye hafla ambayo ilifanyika katika eneo la Ogembo kaunti ya Kisii.
“Ombwoge alikuwa mtu wa kutetea taifa la Kenya kwa kupambana na magaidi kuhakikisha waakazi wanaishi kwa amani bila changamoto na ninampongeza kwa kujitolea wake,” ripoti ya Uhuru Kenyatta ilisema.
“Obwoge ni shujaa kwani alijitolea kuona kuwa wakenya wana upendo, umoja na amani,” aliongeza Kenyatta.
Aidha, generali Walter Ralia aliomba kila Mkenya kuhakikisha mradi wa yumba kumi umepewa kupaumbele ili kupunguza uhalifu nchini.