Mashirika za kutetea haki za kibinadamu katika kaunti ya Kisumu yameshtumu hatua ya rais kuidhinisha rasmi mswada wa usalama 2014 kuwa sheria.
Katika kikao na wanahabari jijini Kisumu, mashirika hayo yanalalama kuwa sheria hiyo mpya inapeana mamlaka zaidi kwa serikali na maafisa wa polisi, huku mwananchi akisalia mmnyonge.
Wakiongozwa na katibu mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Transform Empowerment For Action Initiative George Owour, sheria hiyo mpya inahujumu haki za mwananchi na mashirika yasiyo ya kiserikali, na hata kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shirika la Haki Kenya Hussein Khalid, serikali ya Jubilee inapaswa kuheshimu haki za wakenya na mahakama kushughulikia kufanya kazi kikamilifu.
Naye mwenyekiti wa akina mama kikundi cha Mgombani Alice Obiero amesema sheria hiyo mpya ni kali sana, huku wale watakaoathirika zaidi wakiwa kina mama.