Rais Uhuru Kenyatta akiwahutubia wakaazi wa Kilifi siku ya Alahamisi. Picha/ PSCU.
Rais Uhuru Kenyatta amezindua miradi ya barabara na maji katika Kaunti ya Kilifi iliyogharimu shilingi bilioni Sh3.8.
Barabara hiyo inaunganisha Sabaki, Markebuni, Majengo na Marafa katika gatuzi dogo la Magarini ambalo kwa muda sasa limekuwa likishuhudia tatizo la usafiri hasa majira ya mvua kutokana na barabara mbovu."Tumekuja kutekeleza ahadi tulizozitoa mbeleni, kuhusiana na barabara pamoja na miradi ya kusambaza maji safi, kuhakikisha barabara ziko sawa na huduma ya maji inapatikana kwa urahisi na kila mwanachi katika eneo hili.""Pia tunataka kuwaonesha wanachi kuwa upinzani unapoteza muda kwa kueneza propaganda. Hatutekelezi miradi sababu ya siasa lakini ni kwa sababu tunataka kuboresha miasha ya mwanachi Mashinani,” alisema Rais Kenyatt siku ya Alhamisi wakati wa uzinduzi wa mradi huo.Aidha, Rais pia alikagua mradi wa barabara inayowekwa lami kutoka Kakoneni hadi Salagate unaogharimu shilingi bilioni 4.2.Barabara hiyo inatarajiwa kuinua kiwango cha uchumi katika sehemu hiyo ikizingatiwa kuwa ndiyo hutumika kusafirisha watalii kutoka Malindi na Watamu hadi katika mbuga ya wanyama za Tsavo.Akiandamana na Naibu wa Rais William Ruto, Gavana wa Tana River Hussein Dado, Naibu Gavana wa Kilifi Keneth Kamto, Wabunge Harrison Kombe, Gideon Mung'aro, Mustafa Iddi, Peter Shehe pamoja na Gonzi Rai, Rais aliwataka wananchi kuangalia miradi iliyotekelezwa na Jubilee na kupuuza propaganda za upinzani.