Chama cha Jubilee (JP) kitazinduliwa rasmi mwezi Juni.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kamati andalizi ya chama cha JP ilisema kuwa Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto watakitumia chama hicho kuzitetea nyadhifa zao katika serikali kuu ya kitaifa, wakati wa uchaguzi wa mwaka 2017.

Akizungumza katika mahojiano na radio Citizen siku ya Jumatano, mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo Bwana Dkt Noah Wekesa, alisema kuwa vyama saba vilivyo ndani ya muungano wa Jubilee vimeashiria nia ya kujiunga na JP.

"Kwa wakati huu, maandalizi yote yashakamilika. Rais atazindua chama hichi ifikiapo mwisho wa mwezi Juni au mwanzoni wa mwezi Julai,” alisema Wekesa.

Aliongeza: "Lengo letu kuu ni kumaliza zimwi la ukabila ambalo limeshuhudiwa nchini kwa muda mrefu. Tunataka chama kimoja kisichokuwa na ukabila. Hatutaki kuwarejesha kwa mfumo wa chama kimoja kama miaka ya tisaini sababu ni kinyume cha kipengee 38 cha Katiba huru ya Kenya,” alisema Wekesa.

Vyama hivyo tanzu ni pamoja na TNA, URP, New Ford Kenya, UDF, Agano, APK, GNU na Ford people.