Rais Uhuru Kenyatta atahudhuria sherehe za Madaraka zitakazofanyika katika uwanja wa Afraha mjini Nakuru.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na kamishna wa kaunti ya Nakuru Joshua Nkanatha, tayari afisi ya rais imedhibitisha hayo.

"Kwa sasa tunangojea maafisa wa ikulu kuanza harakati za mipango ya ulinzi," alisema Nkanatha.

Rais Kenyatta amezuru jimbo la Nakuru mwaka huu mara kadhaa na hii itakua mara ya pili ambako kutakua na mkutano mkubwa uwanja wa Afraha baada ya mkutano wa shukrani uliofanyika Aprili 16.

Sherehe hizi zimesemekana kuwa mpango wa Jubilee kumiliki siasa za Bonde la Ufa baada ya chama cha KANU kuonekana kupata umaarufu.