Kamishna wa kaunti ya Nyamira Josphine Onunga amesema kuwa Rais Uhuru Kenyatta atazuru kaunti ya Nyamira na Kisii siku ya Jumatano. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akihutubu kwenye hafla iliyowaleta pamoja washikadau wa idara ya usalama kwenye ukumbi wa makazi ya viwanda KIE mjini Nyamira siku ya Jumatano, Onunga alisema kuwa Rais Kenyatta anatarajiwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika kaunti ya Nyamira. 

"Kesho Rais Uhuru Kenyatta atazuru kaunti ya Nyamira pamoja na ile ya Kisii na anatarajiwa kukagua ujenzi wa barabara ya kilomita 14 katika eneo la Mosobeti- Kebirigo na pia kuzindua rasmi ufunguzi wa hospitali ya level 5 ya Nyamira," alisema Onunga. 

Onunga aidha aliongeza kwa kuwarahi wananchi kujitokeza ili kumkaribisha rais Uhuru Kenyatta atakapozuru kaunti hiyo. 

"Ni ombi langu kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye maeneo atakapozuru Rais Kenyatta ili kumkaribisha kama njia mojawapo yakudhirisha umoja wetu," aliongezea afisa huyo.