Raisi Kenyatta. [Picha/ghafla.com]
Wazee wa vijiji vya maeneo mbali mbali eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale wamemtaka raisi Kenyatta kutimiza ahadi yake ya kuwapa ugavi wa fedha maalumu za wazee zinazotolewa na serikali kila mwezi.
Wakiongozwa na Juma Ali wamesema kwamba rasi Kenyatta aliahidi kutatua kilo hicho wakati alipokuwa akifanya kampeni,lakini hadi sasa bado hajatimiza ahadi yake.
“Tunamtaka raisi atomize ahadi yake aliyotupa wakati wa kampeni zake,hatujasahau”,alisema Ali.
Akizungumza wakati wa sherehe za Jamuhuri,eneo la Msambweni, amemtaka raisi kutimiza ahadi hiyo ili wazee hao waweze kujikimu kimaisha kama wazee wengine.
“Tupewe hizo pesa na sisi tujikimu kimaisha,hali imekuwa ngumu kimaisha,''alisema Ali.
Kwa upande wake naibu kamishna eneo la Diani, Cecili Mutwiri ameahidi kushughulikia swala hilo kwa haraka.
Amewataka wazee hao kutokuwa na hofu kwani serikali inashughulikia swala lao na litatimizwa kwa haraka.
“Raisi hajasahu,bado anakumbuka ahadi yake na ipo siku atawatimizia”,alismea Mutwiri.
Amewataka wazee hao kuwa na subra na matakwa yao yatatimizwa.