Naibu Mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya ardhi nchini Abigael Mbagaya amesema ripoti kamili ya wanyakuzi wa mashamba ya serikali mjini Kisii itatolewa ndani ya majuma mawili yajayo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya kubainika kuwa mashamba mengi ya serikali yamenyakuliwa na watu binafsi ambao baadhi yao ni mabwanyenye katika kaunti hiyo.

Akizungumza mjini Kisii Mbagaya alisema kuwa wakati tume hiyo ya ardhi ilikuwa inafanya uchunguzi kubaini walionyakua mashamba ya serikali na akakiri kuwa walishuhudia changamoto nyingi katika uchunguzi wao huku akisema wote waliogunduliwa kumiliki ardhi kihalifu watashugulikiwa pasi huruma.

“Kwa majuma mawili yajayo tume yetu itatoa ripoti kamili dhidi ya wanyakuzi wa mashamba ya serikali hapa Kisii na wataondolewa katika ardhi hizo mara moja,” alisema Mbagaya.

Wakati huo huo, Mbagaya alisema baadhi ya wanyakuzi hao walijitengenezea hatimiliki za mashamba hayo ya unyakuzi ambazo alisema ni ghushi na sitatupiliwa mbali bila huruma.