Wazazi wote nchini wamehimizwa kuwasomesha wanao ili kujisaidia nyakati zijazo na kujitenga na masuala ambayo hayana usaidizi wowote maishani.
Wito huo umetolewa baada ya serikali kutoa masomo ya bure katika shule za serikali huku wazazi wakitakiwa kutoa usaidizi mdogo ikilinganishwa na hapo wali.
Akizungumza hapo jana katika uwanja wa Nyamache eneo bunge la Bobasi kaunti ya Kisii, Naibu Rais William Ruto aliwahimiza wazazi kuhakikisha wanao wanaenda shuleni ili kujisaidia nyakati zijazo.
“Serikali inaendelea kutoa masomo bila malipo asilimia ndogo ambayo imebaki ni ile ya wazazi nao kutoa kitu kidogo maana serikali inalipia wanafunzi karo nyingi kuliko ile wazazi wanalipa,” alisema Ruto.
“Tunahitaji masomo kupewa kipaumbele katika taifa letu la Kenya maana masomo ndio msingi wa kila jambo katika siku ambazo tumefika,” aliongeza Ruto.
Aidha, Ruto alisema shule zile ambazo bado hazijapata nguvu za umeme, serikali ya kitaifa itajaribu kuziunganishia umeme ili wanafunzi wapate mda wa kusoma kila wakati.
“Hivi karibuni shule zile hazina nguvu za umeme zitakuwa zimeunganishiwa ili masomo yasonge mbele,” alisema Ruto.
Sasa jukumu ni wazazi kuitikia wito wa Ruto na kuwachukua wanao shuleni.