Naibu wa Rais Bwana William Ruto ameiomba jamii ya wakisii kuunga serikali ya JAP mkono, ili kufanikisha maendeleo na kuimarisha uchumi wa nchi.
Bwa Ruto alisema haya kwenye kanisa la Katholik ya St. Antones Marani, katika hafla ya harambee ya kusaidia makanisa ya eneo hilo, ambapo alifunua kuwa serikali ya Jubilee ipo tayari kushirikiana na viongozi wa Kisii ili kuleta maendeleo yatakayowanufaisha wakazi wa kaunti ya Kisii na eneo la Gusii kwa jumla.
“Nawaomba mtuunge mkono kama serikali na tuache kupiga siasa duni, siasa yetu ni maendeleo na kuweka usala kwa watu wetu wote bila kubagua," alisema Ruto huku akiwasuta wanasiasa wa upinzani ambao alisema wanapotosha wakenya.
Naye Gavana wa Kisii, ambaye alihudhuria mchango huo, alimhakikishia kuwa serikali ya kaunti ya Kisii itashirikiana na serikali kuu ili kupigana na jinamizi la ugaidi, ambalo limewaua wanafunzi kule Garissa na wanafunzi wengi kutoka Kisii waliathirika.
“Katika uboreshaji wa usalama kwa jumla, tutajikaza kama kaunti, haswa Kisii ikiwa mojawapo ya zile zilipoteza wanafunzi wetu wengi ili kukomesha ugaidi,” gavana Ongwae aliongezea.
Bwa Ruto alikuwa ameandamana na wabunge Steve Manoti (Bobasi); Kabando wa Kabando (Mukurueni) Jimmy Nuru ( Kitutu Chache North) na viongozi wengine kutoka kaunti ya Kisii wakiongozwa na gavana Ongwae pamoja na naibu wake Bwa Maangi.