Naibu gavana wa Nakuru Joseph Ruto amekanusha madai kuwa serikali ya kaunti ya Nakuru ina deni la shilingi bilioni 2.3.
Rutto amesema kuwa deni linalodaiwa serikali ya kaunti ya Nakuru ni shilingi milioni mia nane, deni ambalo anasema waliridhi kutoka kwa iliyokuwa manispaa ya Nakuru.
"Deni ambalo tunadaiwa ni shilingi milioni mia nane, ambalo ni deni lililoachwa na iliyokuwa manisapaa ya Nakuru kabla ya ugatuzi kuingia," alisema Ruto.
Rutto aliongeza kuwa pesa zinazodhaniwa kuwa deni ni shilingi bilioni 1.8, ambazo ni pesa za kuwalipa wanakandarasi ambao hawajakamilisha kazi.
"Kuna shilingi bilioni 1.8 ambazo ni za kuwalipa wanakandarasi, lakini wengi wao hawajakamilisha kazi lakini pesa zipo na hill si deni," aliongeza naibu huyo.
Naibu gavana huyo alikuwa akiongea Jumanne usiku katika mahojiano katika Radio Citizen.