Naibu wa rais William Ruto amewaonya wakenya kujitenga na wanasiasa wasio na ajenda ya nchi, akisema kuwa serikali ya Jubilee inaskiza marekebisho ya kuleta maendeleo ila si cheche za maneno kutoka kwa wanasiasa wasio na ari ya wakenya.
Ruto aliwaeleza wakenya kuwa macho kwa viongozi wanaosuta serikali kwa kujinufaisha, huku akiwahakikishia wananchi kuwa ahadi ya serikali ya Jubilee itatimizwa.
"Viongozi wa kweli wanatarajia kukosoa serikali kwa niaba ya Wakenya bali si kwa ajili yao, ahadi tuliyowapa kama kuweka umeme kwa shule zote za msingi, ujenzi wa barabara itakamilika," alisema Ruto.
Ruto aliongeza kuwa hakuna kitakachowazuia kutekeleza wajibu wao kama serikali.
Naibu wa Rais alinyasema hayo alipozuru shule ya upili ya Sugoi kaunti ya Uasin Gishu siku ya Jumamosi.