Naibu wa rais William Ruto amesema kuwa serikali itaangalia upya uhamisho wa wafanyikazi wa chuo cha Kenya Medical Training College (KMTC) katika kaunti mabalimbali.
Alionyesha wasiwasi kutokana na sera hizo kwani wafanyakazi wa chuo hicho wameathirika pakubwa.
Ruto alizungumza katika sherehe ya thelathini na tatu ya kuhitimu ambapo mahafala elfu saba walifuzu.
Alisema serikali itashirikiana na taasisi hizo ili kuboresha elimu inayotolewa kote nchini.
"Serikali itatoa shilingi milioni 500 kwa minajili ya kuboresha vifaa vya vyuo mbalimbali," Ruto asema.
Aliongeza kuwa bodi ya kuwapa wanafunzi wa vyuo vikuu mkopo Helb inapanuliwa ili pia kuwasaidia wanafunzi katika taasisi za elimu ya kati.
"Ni jambo la kusikitisha mno ikiwa mwaka uliyopita ni wanafunzi elfu ishirini tu waliofaidika na mikopo hiyo ilhali ilitarajiwa wanafunzi zaidi kuomba au kufaidika kutokana na mkopo huo," aliongeza Ruto.