Nchi ya Rwanda inayoongozwa na Rais Paul Kagame imeukaribisha uamuzi wa Mahakama ya Mombasa wa kutupilia mbali kesi inayohusisha nchi hiyo na mfanyibiashara mashuhuri Salad Awale.
Kesi hiyo ililenga kutathmini mmliki halali wa ardhi ya ekari 32 iliyotunukiwa Rwanda na utawala wa Rais mstaafu Daniel Arap Moi mwaka wa 1986.
Kulingana na ripoti zilizochapishwa katika jarida la East Africa, serikali ya Rwanda imesema itaendeleza mradi wake wa kujenga majumba ya kibiashara kwa kuwa utata huo wa umiliki umetatuliwa.
Mahakama hiyo ikiongozwa na Jaji Anyara Emukule iliamua kuwa hati miliki ya Salad Awale haikuwa ya haki kwa sababu maelezo hayakulingana na maelezo ya mkataba wa hati miliki.
Nchi ya kenya pia ilipewa ekari 32 huko rwanda kama zawadi.
Waziri wa Biashara Rwanda Francois, alisema washatafuta wawekezaji wa kuimarisha sehemu hiyo ya ardhi liyoko karibu na Bandari ya Mombasa.
"Hii ni habari njema na tayari tumefanya uchunguzi wa kina juu ya ardhi hiyo, ili tuweze kuihudumia mali yetu ambayo huwa inaingia katika Bandari ya Mombasa,” alisema waziri huyo.