Shirika la Safaricom limezindua rasmi makao makuu katika eneo la Nyali, mjini Mombasa, hatua inayonuia kusaidia kuimarisha huduma za mawasiliano ukanda mzima wa Pwani.
Akiongea na wanahabari kwenye uzinduzi huo, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bob Collymore alisema kwamba kwa muda mrefu, wakaazi katika ukanda wa Pwani wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi, hatua iliyopelekea wengi wao kusafiri hadi Nairobi.
Collymore alisema kuwa uzinduzi wa afisi hiyo utasaidia kuimarisha zaidi huduma bora miongoni mwa wateja.
Aidha, aliongeza kwamba lengo kuu la afisi hizo nikuona wateja wakinufaika bila kushuhudia matatizo yoyote.
Collymore pia alisema kuwa wanalenga kutoa huduma kwa wateja zaidi ya million 2.2 katika ukanda wa Pwani.
Wakati huo huo, mkurugenzi huyo akisema kwamba mbali na ukanda wa Pwani wanapania kuzindua afisi zengine sawia na hizo katika kanda zingine humu nchini.