Seneta wa kaunti ya Mombasa Hassan Omar ameitaka serikali na wasimamizi wa chuo kikuu cha Nairobi kuwachukulia hatua kali za kisheria wanafunzi waliotekeleza uharibufu wa mabweni na madarasa katika chuo hicho.
Akiongea na wanahabiri mjini Mombasa siku ya Juamatano, Sarai alisema kuwa jinsi wanafunzi wa chuo hicho walivyofanya ni ubadilifu mkubwa wa mali ya umma na shule na lazima sheria kuchukua mkondo wake.
Sarai amesema kuwa madai yaliyosambazwa katika mtandao wa kijamii ya maafisa wa polisi kuwadhulumu na kupiga wanafunzi lazima yachunguzwe na hatua za kisheria kuchukuliwa kwani inaonyesha wazi kuwa katiba ya nchi inakiukwa.
"Tunataka serikali na wasimamizi wa chuo kikuu cha Nairobi kuhakikisha kuwa wanawachukulia hatua kali za kisheria wanafunzi na maafisa wa polisi waliyowadhulumu wanafunzi kwa kuwapiga kwani video iliyotumwa kwa mtandao wa kijamii ulionyesha wazi," alisema Sarai.
Kauli ya Sarai imejiri baada ya wanafunzi wa chuo kuu cha Nairobi kufungwa baada ya kuzuka rabsha kufuatia uchaguzi chuo humo ilidaiwa kuwa na udanganyifu mkubwa.
Picha: Seneta wa kaunti ya Mombasa Hassan Omar. Ameitaka serikali na wasimamizi wa chuo kikuu cha Nairobi kuwachukulia hatua kali za kisheria walioharibu mali ya shule kuadhibiwa.