Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mbunge wa Lugari Ayub Savula ametaka kesi inayowakabili naibu rais William Ruto na mwanahabari joshua arap sang katika mahakama ya kimataifa ya jinai ya ICC kutamatishwa.

Akizungumza mjini Nakuru, mbunge huyo amesema kuwa ana imani kuwa kesi hiyo itakamilika vyema na wawili hao wataachiliwa na kuwa huru.

Licha ya kesi hiyo kuendelea katika mahakama hiyo aliongeza kuwa wakenya wanaendelea kutangamana kwa ajili ya maendeleo humu nchini.

Kando na hayo aliitaka serikali kuweka mikakati kabambe ya kuwapa wakimbizi makaazi ambao hawajapata makao yao na kukamilisha swala hilo.

Alisema ni jambo la aibu pale baadhi ya wakimbizi walifanya maandamano huku kesi inayomkabili naibu rais ikiwa katika mahakama hiyo ya ICC.

Amemtaka rais Uhuru Kenyatta kuandaa mipango ya kitaifa ya maridhiano na utangamano ili kuweka kikomo sintofahamu inayowakumba wakimbizi wa ndani kwa ndani.