Mkurugenzi wa bodi ya utalii hapa nchini Ndegwa Muriithi amesema kwamba sekta ya utalii ingali dhabiti licha ya misukosuko ya kiusalama ambayo inaendelea kushuhudiwa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa hoteli moja mjini Machakos, Muriithi amefichua kuwa Kenya inakumbwa na uhaba wa nyumba za kulala na majumba ya kifahari ya kufanyia mikutano.

Aliwataka Wakenya kuekeza kwenye sekta hiyo, ili kuweka Kenya kiwango cha kimataifa na kuvutia watalii wengi.

Muriithi pia alielezea imani yake kuwa visa vya kigaidi havitaathiri sekta hiyo.

Gavana wa Machakos Alfred Mutua, aliyehudhuria hafla hiyo, alifichua kuwa iwapo sekta ya utalii itaimarishwa humu nchini, basi uchumi wa Kenya utaimarika kwa kiwango kikubwa.

Sekta ya utalii katika nchi ya Kenya imeathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na ugaidi.

Mataifa ya nga'mbo yalitoa taadhari kwa wananchi wake dhidi ya kuzuru Kenya ma maenea flani nchini.

Ikumbukwe kuwa baada ya shambulizi huko Mpeketoni, mahoteli mengi katika mkoa wa Pwani yalifungwa na kupelekea wafanyi kazi wengi wa hoteli kupoteza kazi.

Kenya imo mbioni kurai mataifa ya kigeni kulegeza misimamo yao dhidi ya usafiri nchini, huku mikakati maalum ikizingatiwa ili kulinda sehemu ambazo watalii huzuru kwa wingi.