Siku chache tu baada ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kuzuru maeneo ya Gusii, seneta wa Nyamira Kennedy Mongare amejitokeza kumshtumu rais kwa kutumia mawakala kufahamisha viongozi kuhusiana na ziara yake maeneo hayo. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiwahutubia wanahabari mjini Nyamira siku ya Jumamosi, Mong'are alilalamikia pakubwa hatua ya ofisi ya rais kuwapa viongozi ilani ya siku moja tu kuhusiana na ziara yake.

"Ile miradi yote ambayo rais Kenyatta alizindua hapa kwenye ziara yake ni jambo la busara, lakini kuna wale mawakala ambao wanamleta rais hapa bila kuwafahamisha viongozi, ni jambo mbaya na iwapo rais Kenyatta anataka tufanye kazi naye lazima ajue ya kwamba kuna viongozi waliochaguliwa na wananchi na sharti tupewe heshima," alisema Mong'are. 

Mong'are aidha aliusuta muungano wa Cord kwa kutaka kuiondoa ofisini kwa kufanya maandamano ya kushinikisha tume hiyo kuondoka ofisini. 

"Lazima tukitaka kubandua tume ya IEBC ofisini tutumie sheria ziliopo, na isiwe kwamba tunatumia vurugu ili kuwashinikisha makamishna wa tume hiyo hiyo kuondoka ofisini na sharti wanachama wa Cord waheshimu hilo," alisema Mong'are.