Jamii ya wakisii imeombwa kusubiri ili kuealekezwa mahala watakopopiga kura mwaka ujao wa uchaguzi, baada yao kuwa katika upizani kwa miaka 10 sasa.
Kulinanga na seneta wa Nyamira Kennedy Mongare, jamii hiyo imekuwa 'kwa baridi' sana kwa kuwa mbali na serkali.
"Huu ni mwaka wa kumi sasa tupo katika upizani, bila faida yeyote ilihali kuna maendeo ambayo tunafaa kuyafanya kama tungekuwa serkalini," alisema Mongare.
Seneta huyo alikuwa akihutubia wananchi wa kaunti ya Nyamira, huku akiongeza kuwa viongozi wa jamii ya mkisii watakaa wazungumze na wakubaliane ni wapi pa kupitia.
"Viongozi tutakaa tujadiliane kwa umakini ni vipi tutaweza kuingia serikalini ili tusiwe watu wa kuomba omba kwa serkali, bali jamii ambayo inaweza toa mchango ama kuzungumza na kusikika bila shida yeyote," aliongeza.
Fauka ya hayo, Mongare alisema yeye hawezi kuwa nje ya serikali tena katika uchaguzi mkuu ujao, na kwamba hatatazama walio serikalini wakila keki huku yeye akiwa nje.
Vile vile aliongeza kuwa Rais Uhuru amezindua miradi mingi bila kujali mrengo wa chama alicho mtu binafsi ama msimamo wa jamii kwa mswala ya vyama.