Seneta wa kaunti ya Nyamira Kennedy Okong’o ameiomba serikali ya kaunti hiyo kutumia milioni 47 kununua dawa za hospitali na kukarabati barabara badala ya kutumia pesa hizo kunyunyuzia maji miche ya miti.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya serikali ya kaunti hiyo kutenga millioni 47 katika mradi wa kunyunyuzia miche ya miti maji, huku Okong’o akisema mvua inayonyesha eneo la Kisii inatosha, na kudai hiyo ni njia moja ya kutumia vibaya pesa za wananchi.

Okong’o, aliyezungumza mjini Nyamira alisema pesa za wananchi zinafaa kuwafaidi kimaendeleo, na kuomba gavana wa kaunti hiyo John Nyagarama kusimamisha mradi huo wa unyunyuzaji maji.

“Serikali ya kaunti ya Nyamira ilitenga million 47 katika mradi wa kunyunyuzia maji miche ya miti, naomba pesa hizo zitumike kununulia hospitali dawa ili wagonjwa wafaidike wanapotafuta matibabu,” alipendekeza Okong’o.

“Pesa zingine zitumike kukarabati barabara na maendeleo mengine ambayo ni ya kupendedeza siwezi kubali mamiliioni ya pesa kutumika katika mradi ambao hauna manufaa,” aliapa Okong’o.