Seneta wa kaunti ya Nyamira Kennedy Okong'o amemsuta waziri wa elimu Dkt Fred Matiang'i kwa kusema kwamba vitabu vitanunuliwa kutoka kwa wizara ya elimu.

Share news tips with us here at Hivisasa

"Waziri amepotoka kimaadili na kimawazo kwa kusema kwamba vitabu viwe vukinunuliwa kutoka Nairobi (wizara), ilihali hapa mashinani kuna maduka ya kuviuza vitabu hivyo," alisema Okong'o.

Okong'o aidha alisema kwamba kama vitabu vitanunuliwa kutoka Nairobi, ni kwamba wenye maduka ya vitabu watayafunga maduka hayo na wafanyikazi wafutwa kazi kwa kuwa hamna wanunuzi.

"Matiang'i anamaanisha maduka ya vitabu humu nchini yafungwe na wafanyikazi wote wafutwe kazi kwa kuwa hawana wanunuzi na kwa hivyo hamna pesa za kuendesha shughuli nzima," alisema seneta huyo.

"Hilo jina 'magufuli' wa Kenya linampotosha waziri, Magufuli ilimchukuwa mda kufika kiwango alipo sasa. Matiang'i yamfaa ashauriane na washikadau wengine ili kuleta mabadiliko," aliongeza Okong'o.