Seneta wa Kaunti ya Nyamira Kennedy Okong'o ameitaka serikali ya kaunti kukarabati Hospitali Kuu ya Kaunti ya Nyamira ili kuwahakikishia wenyeji huduma bora.
Akihutubu kwenye uwanja wa Shule ya msingi ya Nyamira, Okong'o alisema kuwa hospitali hiyo ina upungufu wa wahudumu wa afya na madawa, pamoja na nafasi yakutosha ya kuegeza magari.
Okong'o alisema kuwa wagonjwa wengi hulazimika kupanga foleni kwa muda mrefu kabla yakupata huduma za matibabu.
"Nimekuwa nikitembelea Hospitali Kuu ya Nyamira na nimeshuhudia kwamba usajili wa wagonjwa huchukua muda mrefu sana na hamna dawa na wahudumu wa kutosha. Tunahitaji usimamizi wa hospitali hiyo kutenga nafasi yakutosha kwa wagonjwa kujisajili,” alisema Mongare.
Seneta huyo aliisihi bodi yakuajiri wafanyikazi wa umma kwenye Kaunti ya Nyamira kuajiri wahudumu wa afya zaidi kwenye hospitali hiyo, ili kusaidia kurahisisha huduma kwa wagonjwa huku akiongezea kwamba vyumba vya wodi vinastahili kuongezwa hospitalini humo ili kuhimili idadi kubwa ya wagonjwa.