Seneta wa kaunti ya Nyamira kennedy Okong’o ametishia kuzitangaza shule zote ambazo zimekuwa zikiongeza karo ya shule katika kaunti ya Nyamira.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Okong’o alisema atazitangaza shule hizo ambazo zimekuwa zikiongeza karo kwa wanafunzi, jambo ambalo ni kinyume na sheria kwani karo haistahili kuongezwa kamwe.

Akizungumza mnamo siku ya Jumatatu katika eneo la Tombe kaunti ya Nyamira, Okong’o alisema serikali ya kitaifa huwalipia wanafuzi kiwango flani cha karo, na kuongeza kuwa shule zimeongeza karo kupita kiwango atazitaja peupe na kuzitangaza ili kuchukuliwa hatua na serikali kwa kukiuka sheria.

“Kuna baadhi ya shule ambazo hupenda kuvunja sheria kwa kuongeza karo ya shule na ninasema hivi shule zikifunguliwa nitazitaja,” alisema Okong’o.

Wakati huo huo, Okong’o aliwahimza wazazi kushirikiana naye kuhakikisha shule haziongezi karo hiyo huku akiwaomba kuripoti shule ambazo hukiuka sheria hiyo.

Ikumbukwe kuwa serikali kuu ilitangaza kuwalipia wanafunzi karo kwa kiwango flani na hakuna shule inaruhuisiwa kuongeza karo kwa wanafunzi.