Mbunge wa zamani wa Subukia koigi wa wamwere amemkashifu seneta Wa Nakuru James Mungai akisema kuwa hafwatilii jinsi fedha zinavyotumika kwenye kaunti. Akiongea siku ya Jumanne Jijini Nairobi, mwanasiasa huyo alisema kaunti ya Nakuru inahitaji uongozi mpya maana viongozi wa sasa wamefeli.
“Seneta Mungai amefeli wakaazi wa Nakuru. Hajakua kwa mstari wa mbele kufuatilia jinsi kaunti inatumia pesa, yeye amefeli hata kuliko gavana,” Koigi alisema.
Koigi alitangaza azima yake ya kuwania kiti cha useneta wa nakuru kwenye uchaguzi ujao.