Baada ya vikao vya bunge la kaunti ya Nyamira  kusimamishwa kwa wiki mbili zijazo kutokana  na ukosefu wa pesa katika kaunti hiyo ,Seneta wa kaunti hiyo Kennedy Mong’are Okong’o ameingilia kati suala hilo kujua  ni nini kilisababisha kaunti hiyo kukosa pesa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea siku ya Jumatano jioni katika mji wa Nyamira, Seneta huyo alisema kulingana na ripoti alizo nazo kutoka bunge la kitaifa zinaonyesha kuwa  pesa  kaunti ya Nyamira ilipokezwa silikuwa za kiwango cha kutosha kufanya shughuli zote za kaunti hiyo mpaka mwishoni mwa mwaka huu.

Aidha, Okong’o mesema ataendelea kufanya uchungunzi kwa kina na kufuata suala hilo ili kubaini ni nini kilisababisha serikali ya kaunti hiyo kukosa pesa za kuendesha mambo muhimu.

Wakati uo huo ,seneta alighadhabishwa jinsi serikali hiyo hutumia pesa na kumwomba  gavana wa kaunti hiyo John Nyagarama kufuata suala hilo na hata kuelezea jinsi pesa hizo zilitumika.

“Nashindwa kujua jinsi pesa zilitumika katika kaunti hii ya Nyamira ili hali serikali ya kaunti hii ilipokea pesa za kutosha  ambazo zingeendesha shughuli za kaunti mpaka pesa za mwaka ujao,” alisema Okong’o.

Kwa upande mwingine wakaazi wa kaunti hiyo wameshindwa jinsi kaunti hiyo inatumia pesa na kusimamisha shughuli za bunge  

“Sisi tumepoteza imani na wawakilishi wetu wa wadi, spika wa kaunti ya Nyamira Joash Nyamoko akiwa mmoja wao na hata Gavana Nyagarama,” alisema George Obiri mkaazi wa kaunti ya Nyamira.