Seneta wa Kaunti ya Mombasa Hassan Omar amewahimiza vijana kukumbatia elimu ili waweze kujiendeleza kimaisha.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza alipowakaribisha viongozi wa dini ya Kiislamu kutoka Nigeria, India na Burkina Faso katika Kaunti ya Mombasa, kuweka msingi wa kujengwa kwa Chuo Kikuu cha Kisheria katika eneo la Makinnon, Kaunti ya Kwale, Omar alitoa wito kwa vijana wa Kiislamu kukumbatia elimu ili kupata ujuzi, kuelewa dini vizuri na kuwa na ushindani katika jamii.

Seneta huyo aidha alitoa wito kwa vijana wa Kiislamu ambao wamejiunga na vikundi ya kigaidi nje ya nchi kurudi nyumbani.

"Huwezi kuwa Muislamu kama hujasoma kwa sababu huwezi kujua nini unatakikana kuliombea. Dini ya Kiislamu ni dini ya amani ambayo inadhihirisha elimu. Sisi tunatambuliwa kama wasomi kutoka nyakati za kale na wala sio wauaji,” alisema Omar.