Seneta wa Nairobi Mike Sonko amekosa kuhudhuria kikao cha mahakama kuelezea aliko mwenyekiti wa vuguvugu la MRC, Omar Mwamnuadzi.
Siku ya Jumatatu, mahakama ilitoa agizo jipya la kumtaka seneta huyo kufika mbele ya mahakamani, baada ya wakili wake, Jerad Magoloo, kuambia mahakama kuwa Sonko hajapewa agizo lolote la kumtaka kufika mbele ya Mahakama ya Mombasa.
Kufikia sasa, Omar Mwamnuadzi amesusia vikao vitano vya kesi zinazomkabili.
Mwamnuadzi na wenzake zaidi ya 20 wanakabiliwa na mashtaka ya kuandaa mkutano kinyume cha sheria na kuwa wanachama wa kundi la MRC.
Majuma mawili yaliyopita, Idara ya polisi katika Kaunti ya Kwale iliagizwa kumtia mbaroni mwenyekti huyo kwa kususia vikao vya kesi inayomkabili.
Seneta Sonko ndiye mdhamini wa Mwamnuadzi.
Kesi hiyo itatajwa tena Septemba 23, 2016.