Seneta wa kaunti ya Nyamira Mong’are Bw’okongo amesema kuwa ufisadi unafaa kutangazwa kuwa janga la kitaifa kwa kuwa umesambaa kote.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hii imeweka kwenye shauku imani ya wakenya aitha kwa wabunge au kitengo cha kupambana na ufisadi nchini Kenya.

Seneta alikuwa akiyasema haya wakati alipoitembelea hospitali ya Nyamira kufanya majadiliano na halmashauri simamizi ya hospitali hiyo kuhusiana na matakwa yao na mapendekezo ambayo bunge la senate litashughulikia kulainisha utoaji wa huduma za afya kote nchini.

Kiongozi huyo wa kaunti alisema kuwa ugatuzi ambao nia yake ulikuwa kuwasaidia wakenya kufikia keki ya kitaifa inapogawanywa umegeuka kuwa jinamizi ya ufisadi mkubwa ambao upo kutoka mashinani hadi kitaifa.

“Angalia bunge na tume ya Namwamba. Ni ufisadi wa kula hela za wananchi kwa kushiriki ulaji wa hongo kiholelaholela,” alisema kiongozi huyo.

Pia alimtaka Ababu Namwamba kuubeba msalaba wake mwenyewe kwani hata mahakamani atashtakiwa yeye.

Kuhusiana na swala ambapo magavana walidinda kushiriki utoaji wa mitambo ya kiafya na rais Uhuru Kenyatta, Okong’o aliwalaumu magavana kwa kuingisha ubinafsi kwa mpango huo mzuri na wa kupiga hatua kwa kuwatibu wagonjwa kote nchini.

“Ni jambo la kusikitisha sana kuwaona magavana wakiendeleza ubinafsi wao kwa maswala nyeti kama afya,kwa hili hawana budi ila kusalimu amri na kushirikiana na rais kwa mpango huu wa afya utamnufaisha mwananchi,” aliendelea kusema.

Aliahidi mipangilio ambayo kamati ya afya katika senate kama ambayo itarahisisha utoaji wa huduma kwa mujibu wa kaunti mbalimbali kama kupitisha mswada wa kuongeza hela ambazo zitafadhili mipango ya maendeleo kiafya.