Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Seneta wa kaunti ya Bomet Wilfred Lesan amesema kuwa uchaguzi mdogo wa Kericho ulikuwa huru na wa haki na hakukua na visa vyovyote vya wizi katika uchaguzi huo.

Akizungumza na wanahabari kaunti ya Mombasa baada ya mkutano baina ya maseneta na wizara ya ugatuzi, Lesan aliipongeza tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka IEBC kuwa iliandaa uchaguzi huo kwa njia inayofaa.

Wakati huo huo seneta huyo alitoa tahadhari kwa gavana wa kaunti ya Bomet Issac Ruto kuwa atawasilisha hoja kwa kamati ya fedha katika bunge la seneti ili afanyiwe udadisi jinsi alivyotumia fedha za kaunti katika uchaguzi huo.

Haya yanajiri wakati ambapo wanachama wa KANU wakiongozwa na seneta wa Baringo Gedion Moi walisema kuwa mrengo wa Jubilee ulishirikiana na IEBC kuiba uchaguzi huo.