Seneta wa kaunti ya Nyamira amekashifu mauaji yaliyotekelezwa katika wadi hiyo ya Bokeira mnamo siku y Ijumaa. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Seneta huyo ambaye alitembea kwa marehemu mzee Kamonde alikashifu kitendo hicho kilichotekelezwa katika wadi hiyo kuwa ni cha unyama. 

"Sijawahi kushuhudia kitendo cha kinyama kama hiki maishani mwangu, yaani binadamu aliye na uhai kuchomwa na kemikali ya sumu," alisema seneta Okong'o aliyeonekana kuwa na huzuni nyingi. 

"Ni lazima hawa magaidi waliotekeleza mauaji haya wasakwe na kutiwa mbaroni na wachukuliwe hatua kali na serikali iongeze zaidi maafisa wa polisi katika eneo hili ndio waweze kukabiliana na magaidi hawa," aliongezea seneta huyo.