Saa chache tu baada ya watu kumshambulia seneta wa kaunti ya Nyamira kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na matamshi yake dhidi ya mrengo wa Cord, sasa seneta huyo amejitokeza kuyatetea matamshi yake. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kwenye mahojiano kwa njia ya simu siku ya Jumanne, seneta Okongo aliwasuta vikali baadhi ya watumizi wa mitandao ya kijamii kwa kumhusisha na mrengo wa Jubilee. 

"Inashangaza kwamba baadhi ya wafuasi wangu wanaotumia mtandao wa kijamii wa whatsapp wanaweza nihusisha na serikali ya Jubilee eti kwa sababu kwamba nimetaja wazi kwamba yafaa muungano wa Cord usitishe maandamano dhidi ya IEBC," alishangazwa Mong'are. 

Mong'are aidha alisitisha ya kwamba njia ya kipekee ya kusuluhisha tofauti zilizoko baina ya muungano wa CORD na tume ya IEBC ni kufanyika kwa majadiliano ya pamoja na washikadao.

"Kilicho wazi ni kwamba wakenya wengi hawana imani na tume ya uchaguzi nchini IEBC, ila njia ya kipekee ya kusuluhisha tofauti zilizoko baina ya IEBC na CORD ni kufanyika majadiliano," aliongezea Mong'are.