Seneta wa kaunti ya Nyamira Okong'o Mong'are amejitokeza kuwarai wakristo kuliombea taifa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu ujao. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akihutubu kwenye kanisa la Kiadventista la Kenyenya kwenye eneo la uwakilishi wodi ya Bonyamatuta kaunti ya Nyamira siku ya Jumamosi, Mong'are alisema kuwa yafaa wakristo wawaombee wanasiasa. 

"Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu ujao, ombi langu kwa wakristo kote nchini ni kutuombea sisi wanasiasa ili kusambaza jumbe za amani kwenye kampeni zetu kwa kuwa hatuhitaji kuona uhasama baina ya wakenya wa kabila mbalimbali," alisema Mong'are. 

Mong'are aidha alimpa changamoto rais Uhuru Kenyatta kuhakikisha kuwa waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007 wamefidiwa. 

"Rais Kenyatta alipofanya ziara yake huku Nyamira alisema wazi kwamba waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi watafidiwa kabla ya uchaguzi mkuu ujao na nichangamoto yangu kwake kuhakikisha kuwa waathiriwa hao wamefidiwa kwa wakati," aliongezea Mong'are.