Senata wa kaunti ya Nyamira Mong'are Okongo amewataka wanafunzi kutoka eneo la Gusii kutia bidii masomoni ili kujiimarisha kimaisha. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akihutubu kwenye shule ya upili ya Marindi wakati wa hafla ya kuwapokeza zawadi wanafunzi waliotia fora kwenye mtihani wa kidato cha nne mwaka jana siku ya Jumapili, Mong'are aliwarahi wanafunzi kutia bidii masomoni ili kubadilisha hali yao ya kimaisha. 

"Wazazi wenu huangaika sana kuhakikisha kwamba wamewalipia karo ya shule, na sasa ni wajibu wenu kuhakikisha kuwa mnatia bidii masomoni ili kujistawisha kimaisha," alisema Okong'o. 

Okong'o aidha aliwarahi wanasiasa dhidi ya kuingilia masuala ya usimamizi wa shule za umma huku akihoji kuwa hali hiyo hudhoofisha viwango vya masomo shuleni.

"Ni ombi langu kwa wanasasia wenzangu kujiepusha na mazoea ya kuingilia masuala ya usimamizi wa shule kwa maana hali hiyo huchangia sana katika kurudisha nyuma viwango vya elimu nchini," aliongezea Okong'o.