Wakulima wa mifugo na wale wa mimea katika Kaunti ya Kisii wako na kila sababu ya kutabasamu  baada ya serikali ya kaunti hiyo kusema wataanzisha simu ya kupiga bila malipo  ili kushughulikia shida inapotokea kwa wakulima hao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea na wanahabari katika mji wa Kisii siku ya Jumatano waziri wa kilimo katika kaunti ya Kisii Vincent Sagwe alisema serikali ya kaunti imeweka mikakati kabambe ya kuanzisha simu ambazo wakulima watakuwa wakipiga jambo mbaya linapotokea ili maafisa wa kilimo kujulishwa na  kulishughulikia haraka iwezekanavyo.

Wafugaji wa Ng’ombe, Mbuzi na mifugo wengine watafaidika pakubwa na mpango huo.

“Tukianzisha simu hiyo wafugaji watakuwa wakipiga simu bila kulipishwa malipo yoyote na kumjulisha  afisa husika shida  ambayo amekabiliana nayo ili kushughulikiwa,” alihoji Sagwe waziri wa kilimo kaunti ya Kisii.

“kama ni ng’ombe amekuwa mgonjwa afisa anakimbia anaishughulikia haraka ikilinganishwa na hapo mbeleni maana mkulima alikuwa anasumbuka kumtafuta daktali na watu wamekuwa wengi simu itakuwa ikirahisisha mambo hayo sana,” aliongezea Sagwe.

Wakati huo huo, waziri huyo alisema kuwa seikali ya kaunti ya Kisii itawaajiri maafisa wa  kushughulikia mambo hayo kwa kila wadi zote ambazo ziko katika kaunti ya Kisii.

“Tumepanga jinsi ya kuwaajiri maafisa hao ukiangalia wengi wamezeeka na  wako katika devisheni na katika wilayani sasa tutawatuma katika kila wadi s hivi karibuni ili wakaazi wa kaaunti ya Kisii kunufaika na huduma hiyo,” alidokeza Sagwe.